Bondia Thomas Mashali amekutwa amekufa usiku wa kuamkia leo maeneo ya kimara jijini Dar es salaam kutokana na sababu ambazo hazijajulikana mpaka sasa.

Kwa mujibu wa katibu mkuu wa Oganization ya ngumi za kulipwa nchini PST, Antony  Lutta amesema kuwa taarifa walizozipata ingawa bado hazijathibitihswa ni kwamba marehemu Mashali inasemekana kulikuwa na ugomvi kati yake na mtu (ambaye hakutajwa jina lake) aliyekuwa akidaiana fedha (kiasi hakikutajwa).

Lutta ameongeza kuwa sababu nyingine inayosemekana ni kwamba marehemu enzi za uhai wake amekuwa na tabia ya kufanya vurugu akiwa amelewa na mwili wake umekutwa maeneo ya kimara jijini dare s salaam ukiwa na majeraha ambapo ulichukuliwa na kupelekwa kuhifadhiwa katika  hospitali ya taifa muhimbili.

Marehemu Mashali kabla ya kifo chake alikuwa  acheze na bondia Chimwemwe kutoka nchini Malawi pigano ambalo lilipangwa kufanyika mkoani  morogoro.

Mashali amezaliwa septemba 09 mwaka 1989 ameacha rekodi ya kushinda mapambano 19 kati ya hayo 9 akishinda kwa KO amepoteza mapambano 5 kati ya hayo amepigwa kwa KO mapambano 4 huku akitoka sare pigano moja tu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *