Baba mzazi wa aliyekuwa mbunge wa viti maalum, marehemu Amina Chifupa, Mzee Hamiss Chifupa amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Upanga, jijini Dar es Salaam.

Taarifa kutoka ndani ya familia ya mzee Chifupa zinasema mzee huyo alikuwa akisumbuliwa na tatizo la kiharusi lililompata toka wiki iliyopita, ambapo alipelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kutolewa mapema wiki hii baada ya kupata nafuu.

Mdogo wa marehemu Rashid Issa amesema kuwa “Baada ya kumtoa Muhimbili tulimpeleka kwa mwanaye wa kike Upanga na jana majira ya jioni alianza kulalamika kuwa hapumui vizuri na majira ya saa mbili za usiku tukiwa katika harakati za kumpeleka hospitali alifariki dunia,”.

Pia ameongeza kwa kusema kuwa “Taratibu za mazishi bado zinaendelea hapa nyumbani kwake Mikocheni ‘B’ na tamko kuwa tutazika lini litatoka baada ya watoto wake waliyopo nje ya Dar es Salaam kufika msibani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *