Tanzania imeshuka nafasi 11 kwenye viwango vya soka vilitolewa leo na shirikisho la soka duniani (FIFA) ambapo imeshika nafasi ya 136.

Katika viwango hivyo, timu ya taifa ya Ujerumani imeshika nafasi ya kwanza ikifuatiwa na timu ya taifa ya Brazili iliyokamata nafasi ya pili.

Tanzania inashikilia nafasi ya 136 sasa baada ya kushuka nafasi 11, Kenya nayo imeshuka nafasi 14 hadi nafasi 102.

Katika mechi za kirafiki ambazo Harambee Stars walicheza hivi majuzi, walilazwa 1-0 na Thailand baada ya kuchapwa 2-1 na Iraq mjini Basra.

Burundi imesalia nafasi ya 129, Uganda ikapanda hatua moja hadi nafasi ya 70.

Malawi imeshuka nafasi moja hadi nambari 117 ambapo inafuatwa katika nafasi ya 118 na Rwanda ambao bado walishikilia nafasi hiyo katika orodha iliyotangazwa awali.

Kwa Afrika  nchi ya Tunisia wanaongoza kiwa nafasi ya 28 duniani baada ya kupanda hatua 3 wakifuatwa na Misri walio nafasi ya 30 duniani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *