Yanga  imefufua matumaini ya kufuzu nusu fainali ya kombe la Shirikisho Afrika baada ya kushinda  1-0 dhidi ya MO Bejaia ya Algeria kwenye mechi iliyofanyika katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Goli pekee la Yanga limefungwa na Amissi Tambwe katika dakika ya pili ya kipindi cha kwanza baada ya Simon Msuva kuunganisha faulo iliyopigwa na Juma Abdul na Tabwe kumalizia mpira huo.

 Ushindi huo unaifanya Yanga ifikishe pointi nne baada ya hapo nyuma kufungwa mechi tatu na kutoa sare moja.

TP Mazembe inaongoza Kundi A ikiwa na alama 10 baada ya mechi nne, ikishinda mechi tatu na kutoa sare moja huku MO Bejaia na Medeama kila moja ina alama.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *