Banda la utalii la Tanzania kwenye maonyesho ya Kimataifa ya ITB yanayoendelea Berlin nchini Ujerumani yamekuwa kivutio kikubwa kwa wageni wanaotembelea maonyesho hayo.

Banda hilo linavivutio mbali mbali kama vile michoro ya nyayo za watu wa kale (Zamadamu), Michoro ya Mlima Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro pamoja na wanywama wanhama katika hifadhi ya Serengeti.

Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania, Devotha Mdachi amesema kuwa pamoja nautangazaji mbali mbali wa vivutio vya utalii vya Tanzania unaofanywa kwenye maonyesho hayo TTB imeamua kuweka mkazo kwa kutangaza Tanzania kama chimbuko la binadamu wa kale.

Jumla ya makampuni 61 kutoka taasisi za uma na binafsi kutoka Tanzania zinashiriki maonyesho hayo ya ITB chini ya usimamizi wa TTB.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *