Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo raia wake hawana furaha dunia kulingana na ripoti iliyotolewa hivi karibuni.

Rwanda iko nafasi ya 151 , Tanzania nafasi ya 153 huku Burundi ikiwa nafasi ya 154 kati ya nchi 155.

Norway ndiyo imechukua nafasi ya kwanza kama nchi yenye watu walio na furaha zaidi duniani, kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa na kumshinda jirani wake Denmark, ambayo ichukua nafasi ya kwanza mwaka uliopita.

Denmark, Iceland, Uswisi na Finland zinachukua nafasi tatu za kwanza huku nchi ya Jamhuri ya Afrika ya katika ikichukua nafasi ya mwisho kati nchi zenye watu wasio na faraha duniani.

Mataifa ya magharibi mwa Ulaya na Marekani pia nayo yako na watu wenye furaha duniani wakati Marekani ikichukua nafasi ya 14 na Uingereza nafasi ya 19.

Nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara na zile zinazokumbwa na mizozo, zina alama za chini.

Syria ilichukua nafasi ya 152 kati ya nchi 155 huku Yemen na Sudan Kusini, nchi zinazokumbwa na njaa zikichukua nafasi za 146 na 147 mtawalia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *