Mchekeshaji maarufu nchini Marekani, Charlie Murphy amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 57.

Charlie amefariki jana Jumatano asubuhi katika hospitali ya mjini New York kutokana na ugonjwa wa leukemia.

Charlie ambaye ni kaka wa mchekeshaji Eddie Murphy amamewahi kuigiza kwenye filamu takribani 29 huku filamu yake ya mwisho kuonekana ilikuwa ni ‘Meet The Blacks’ iliyotoka mwaka jana.

Lakini pia amewahi kushiriki katika uandishi wa baadhi ya filamu za mdogo wake Eddie Murphy ikiwemo “Norbit” na “Vampire in Brooklyn.”

Muigizaji huyo amefanikiwa kupata watoto watatu ambapo wawili kati yao alizaa na mkewe Tisha Taylor aliyefariki Disemba mwaka 2009 kwa ugonjwa wa kansa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *