Aliyewahi kuwa meya wa Dar es Salaam na mbunge wa Afrika Mashariki, Dr Didas Massaburi amefariki dunia katika hospitali ya taifa Muhimbili mahali alikokuwa akipata matibabu yake.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na ndugu yake Makongoro Mahanga ambaye alieleza kuwa familia ipo katika taratibu za awali za msiba huo na leo watatoa ratiba na taratibu nyingine za msiba huo.

Wiki iliyopita Dk Didas Masaburi alilazwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili akipatiwa matibabu mpaka umauti ukamkuta hospitalini hapo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *