Shirika la umeme nchini TANESCO limesema kuwa bei ya umeme itapandishwa kwa watumiaji wakubwa na halina mpango wa kupandisha bei za umeme kwa watumiaji wadogo kama inavyosemwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Mhandisi Felchesmi Mramba amesema kuwa hakuna haja ya wananchi kuwa na wasiwasi kuhusu mapendekezo yaliyo wasilishwa na mamlaka ya udhibiti wa huduma Za nishati na maji EWURA.
Mramba amesema kuwa Niwatoe hofu wananchi kwamba yale mapendekezo tuliyoyapeleka wananchi wa kawaida wale wanaotumia umeme mdogo bei zao hazitaathirika sana. Kuna jambo moja ambalo tumelitazama kwa mtazamo tofauti, unajua sasa hivi we mteja wa kawaida unalipa sawasawa na kampuni zinazoweka mabango barabarani ambazo ni kampuni za kibiashara.
Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji EWURA iliwasilisha mapendekezo ya kupandishwa kwa umeme kwa shirika la umeme nchini Tanesco.