Tamthilia ya Jumba la Dhahabu iliyopata umaarufu miaka ya nyuma inatarajiwa kuoneshwa tena kupitia runinga ya TBC kama ilivyokuwa hapo awali.

Mkurugenzi wa Shirika la Habari Tanzania (TBC), Ayub Rioba amesema wanatarajia kuanza kurudia kuonesha tena tamthiliya hiyo kutokana na maoni ya watazamaji wa shirika hilo.

Amesema mchezo huo ambao unatarajiwa kuanza kuoneshwa wiki ijayo, ambao utakuwa ukioneshwa mara tano kwa wiki ili kuwapa nafasi watazamaji ambao kipindi cha nyuma hawakubahatika kuuona.

Rioba pia alizindua muswada mpya wa tamthiliya ya Ukurasa Uliofungwa ‘Closed Chapter’ ambayo inatarajiwa kuoneshwa katika kituo hicho baada ya kufanyika usaili.

Kiongozi na mtunzi wa filamu ya Jumba la Dhahabu na Kurasa Uliofungwa ‘Closed Chapter’, Tuesday Kiangala, amesema amekubali kuirudisha tamthiliya hiyo kwakuwa alikuwa akiulizwa maswali mengi juu ya tamthiliya hiyo.

Katika tamthiliya ya Jumba la Dhahabu kuna waigizaji waliofanya vizuri kama, Mzee Chilo, Joan, Badboy, Tuesday Kiangala, Capto Rado na Niva wengine wengi.

Tamthilia ya Jumba la Dhahabu ilijipatia umaarufu nchini miaka ya nyuma kutoakana na maudhui ndani ya Tamthilia hiyo iliyoandaliwa na kundi la Fukuto Arts Group.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *