Klabu ya Yanga imeshinda 2-0 dhidi ya Prisons kwenye mechi ya ligi kuu Tanzania Bara katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Yanga wamepata bao la kwanza kupitia kwa Amiss Tambwe katika dakika ya 70 kwa kichwa akimalizia kazi nzuri iliyoanza kwa Chirwa kisha Msuva.

Bao la pili kupitia limefungwa na Chirwa ambaye amemalizia pasi nzuri ya kichwa kutoka kwa Tambwe ambaye naye alipata mpira kutoka kwa Haji mwinyi.

Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika timu hizo zilikuwa bila bila lakini Yanga ilionekana kulitawala lango la Prisons.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *