Mshambuliaji wa Yanga, Amis Tambwe amesema siri ya kuendelea kutikisa nyavu katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara bila kushuka ni kwa vile amekuwa hasikilizi maneno ya mashabiki uwanjani.

Amesema mchezaji yeyote kama anahitaji kufanikiwa na kufanya vizuri katika ligi hiyo hapa nchini hana budi kuziba masikio ya mashabiki na kufanya kile ambacho kimemleta katika timu vinginevyo ni rahisi kupotea.

Tambwe hivi karibuni aliifungia bao timu yake katika mchezo dhidi ya Simba, ingawa inadaiwa kabla ya kufunga aliushika kwa mkono mpira huo.

Mshambuliaji huyo sema anawajua mashabiki wengi wa soka wamekuwa ni wazungumzaji, na kwamba kama angekuwa anawafuatisha angekuwa ameshuka kiwango.

Tambwe tangu kujiunga na Simba msimu wa mwaka 2013 na msimu uliopita Yanga, amekuwa akizidi kuonesha ubora wake katika kufumania nyavu huku msimu uliopita akiibuka kuwa mfungaji bora.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *