Tamasha la Sanaa na Maonesho ‘siku ya msanii’ linatarajiwa kufanyika Septemba 24 mwaka huu katika kijiji cha Makumbusho kilichopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Siku hiyo ni maalumu kwa ajili ya kuenzi kazi zinazofanywa na wasanii mbali mbali katika sanaa tofauti ili kukuza na kuendeleza sanaa nchini ili kufikia malengo.

Katika siku hiyo ya msanii kutakuwa na maonesho mbali mbali ya kazi za sanaa ambazo ni Maonesho ya Jukwaani, Muziki, Ngoma za Asili, Filamu, Sanaa za Ufundi na Muziki wa Injili.

Siku hiyo ya msanii imedhaminiwa na Haak Neel Productions (T) Limited kwa kushirikiana na Barazaa la Sanaa la Taifa (BASATA).

Mashabiki wanaombwa kujitokeza kwa wingi kwenye siku hiyo ili kushuhudia kazi mbali mbali zinazofanywa na wasanii tofauti, na hakutakuwa na kiingilio kwenye tamasha hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *