Shambulizi la bomu limetokea katika viwanja vya makazi ya wakandarasi wa kigeni nje ya mji mkuu wa Afghanistan, Kabul karibu na kikosi cha anga nchini humo kilichoko karibu na mji wa Bagram.

Gari lililokuwa limebeba vilipuzi, linaarifiwa kuripuka katika eneo la karibu na upande wa lango la kaskazini la viwanja hivyo  shambulio ambalo linafanana na lililotukia miaka mitatu iliyopita.

Mara baada ya shambulio hilo tayari waasi wa Taliban wametoa tamko la kukubali kuhusika na shambulio hilo, na kwamba wapiganaji wao wamekuwa wakishambulia kuelekea katia vinja hivyo.

Mpaka sasa hakuna tamko lolote kutoka katika serikali ya Afghanstan na pia hakuna maelezo zaidi kuhusiana na majeruhi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *