Taratibu za talaka kati ya Khloe Kardashian na mpenzi wake Lamar Odom zimekamilika miaka mitatau baada ya Khloe kuanzisha mpango huo.

Kloe mwenye umri wa miaka 32 alianzisha taratibu za kudai talaka hiyo mnamo mwezi Disemba 2013 baada ya wawii hao kuwa katika ndoa kwa miaka minne.

Lakini aliisimamisha taratibu za talaka hiyo baada ya Lamar Odim kupatikana katika mgahawa mmoja akiwa hana fahamu mwaka jana.

Khloe amesema kuwa hali yake ya kiafya ndio sababu moja ya kusitisha talaka hiyo.

Lakini aliendeleza talaka hiyo mnamo mwezi Mei akisema kuwa wameshindwa kuelewana katika ndoa yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *