Hatimaye Kipindi cha Take One cha Clouds TV kinatarajiwa kurudi hewani mwezi huu baada ya  kumalizi kifungo kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) iyotolewa Octoba mwaka jana.

Mamlaka ya Mawasilano Tanzania ilikifungia kipindi hiko kutokana na kukiuka kanuni za utangazaji za mwaka 2005 baada ya kuonyesha kipindi kilichokua kinahamasisha biashara ya ngono ambapo ni kuingilia mambo ya siri ya mtu.

Mtangazaji wa kipindi hicho mahususi kwa masuala ya movie za Kibongo, Zamaradi Mketema ametangaza ujio wa kipindi hicho huku akiwataka mashabiki wa kipindi hicho kutoa maoni juu ya mabadiliko ya kipindi hicho.

Kupitia akaunti yake ya Instagram Zamaradi Mketema ameandika “Tukiwa tumemaliza likizo yetu tuliyopewa na TCRA, kipindi chetu kinarudi rasmi January hii 2017 namaanisha Take One mtangazaji wako nikiwa yuleyule Zamaradi H. Mketema,”.

Sababu ya kipindi hicho kufungiwa miezi mitatu na Mamlaka ya Mawasilano (TCRA) ni mahojiano kati ya mtangazaji wa kipindi hicho Zamaradi Mketema na Gift Stanford Maarufu kama ‘Gigy Money’ na yaliyorushwa Agost 09 saa 3.00 usiku na kurudiwa kesho yake saa 7.00.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *