Taifa Stars imeshuka kwenye orodha ya viwango vya soka vilivyotolewa leo na shirikisho la soka duniani FIFA.

Taifa Stars imeshuka kwa nafasi tano na kufikia nafasi ya 125 wakati kwa ukanda wa Afrika Mashariki Harambee Stars nayo imeshuka nafasi sita hadi nafasi ya 88 duniani.

Nchi zilizopanda katika ukanda huu wa Africa Mashariki ni Rwanda ambao wamepanda kwa nafasi moja, Uganda wamepanda nafasi mbili na wanashikilia nafasi ya 71 na pia Burundi wamepanda nafasi tatu hadi nafasi ya 129.

Ujerumani wamerudi tena kuchukua nafasi ya kwanza huku Brazil waliokuwa wakishika nafasi ya kwanza sasa wamekuwa nafasi ya pili. Ureno waliokuwa nafasi ya sita sasa wako nafasi ya 3 na Argentina waliokuwa nafasi ya 3 wameshuka hadi 4.

Kwa upande wa kumi bora za Africa, Misri wanaongoza wakifuatiwa na Tunisia huku Senegal wakiwa katika nafasi ya 3, ya 4 ikienda kwa DRC.

Nigeria wako nafasi ya 5 wakifuatiwa na mabingwa wa Africa timu ya taifa ya Cameroon huku Burkina Fasso wakishika namba 7, 8 ni Ghana, 9 Ivory Coast na 10 ni Morocco.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *