Shirikisho la soka duniani (FIFA)  limetangaza orodha mpya ya viwango vya kila mwezi kwa timu za mataifa yote duniani.

Timu ya Argentina inaendelea kushika namba moja kwa timu bora zaidi duniani huku ikiwa na pointi 1585 ikifuatiwa na Ubelgiji (1401), Colombia (1331), Ujerumani (1319) na nafasi ya tano imechukuliwa na Chile yenye pointi 1316.

Kwa upande wa nchi za Afrika timu ya taifa ya Algeria inaongoza ikiwa nafasi ya 32 huku ikiwa na pointi 781 ikifuatiwa na Ghana, Ivory Coast na Senegal ikishika nafasi ya nne katika orodha hiyo.

Taifa Stars imeshuka kwa nafasi moja kutoka 123 mpaka nafasi ya 124 na imefanikiwa kupata pointi 300 ikishika nafasi ya tano kwa nchi za Afrika Mashariki ikiongozwa na Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *