Taifa stars imehitimisha mechi za Kundi G kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa kufungwa bao 1-0 na wenyeji Nigeria jioni ya leo Uwanja wa Uyo Akwa Ibom.

Bao pekee la Super Eagles limefungwa na mshambuliaji wa Manchester City, Kelechi Iheanacho dakika ya 78 katika mchezo uliokuwa mkali na wa kusisimua.

Stars ingebugizwa mabao mengi leo kama si jitihada za kipa wake, Aishi Manula kuokoa michomo mingi ya hatari.

Kwa matokeo hayo, Eagles inamaliza nafasi ya pili kwa pointi zake tano, nyuma ya Misri walioongoza kundi na kufuzu AFCON mwakani Gabon, wakati Stars iliyomaliza na pointi moja imeshika mkia.

Misri iliyovuna pointi 10, imefuzu kiulaimi hususan baada ya Chad kujitoa katika kundi hilo katika ya mechi za kufuzu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *