Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imeshindwa kutamba nyumbani mbele ya Rwanda baada ya kulazimishwa bao 1-1 katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Rwanda ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika 18 ambapo Stars walisawazisha dakika 34 kupitia nahodha Himid Mao Mkami.

Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika timu hizo zilikuwa 1-1 na maokeo hayo yamedumu mpaka dakika 90 ya mchezo huo.

Taifa Stars imeonekana kulishambulia lango la Rwanda lakini juhudi zao hazikuzaa matunda na kulazimishwa suluhu ya moja moja.

Timu hizo zinatarajia kurudiana wiki ijayo nchini Rwanda ikiwa ni mechi ya marudiano ya kombe la Chan.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *