Taifa Stars inatarajiwa kucheza na Ethiopia katika mechei ya kirafiki itakayofanyika jijini Adis Ababa Oktoba 8 mwaka huu.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa atakuwa na nafasi ya kuandaa kikosi chake kuanzia Oktoba 3, 2016 mara baada ya michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambako Mwadui itacheza na Azam huku Mbao ikishindana na JKT Ruvu Oktoba 2, mwaka huu kabla ya kupisha kalenda hiyo ya FIFA ya michuano ya kimataifa.

Matokeo ya mchezo huo, ni sehemu maalum ya kupima viwango vya ubora na uwezo wa timu za taifa.

Kwa sasa Tanzania inashika nafasi ya 132 kati ya nchi 205 wanachama wa FIFA zilizopimwa ubora huku Ethiopia ikishika nafasi ya 126.

Katika Bara la Afrika, Ivory Coast ambayo ni ya 34 kwa ubora duniani ndiyo inayoongoza ikifuatiwa na Algeria, Senegal, Tunisia na Ghana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *