Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kinatarajia kuondoka leo kuelekea Rwanda kwa ajili ya kuikabili timu ya taifa hilo, Amavubi.

 Taifa Stars itatokea Mwanza na kuunganisha safari ambapo ikitua Dar, itapanda ndege ya Shirika la Rwanda Air kuelekea huko.

 Taifa Stars inatarajia kurudiana na Amavubi Jumamosi ijayo ya Julai 22, badala ya Jumapili ya Julai 23, mwaka huu kama ilivyokuwa imepangwa awali kufuatia wenyeji wao hao kuwataarifu Caf kuwa mchezo huo uchezwe Jumamosi.

 Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Afred Lucas, amesema wamepata taarifa kutoka Caf juu ya mabadiliko ya mchezo huo ambapo mwalimu amelazimika kubadili ratiba ya siku moja na kikosi kuondoka nchini leo kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *