Mwanamuziki wa hip hop nchini Marekani, Swae Lee amesema kuwa ameamua kuachana na ndoto za kuwa kimapenzi na binti wa Barack Obama, Malia Obama.

Swae Lee amesema kwamba safari ya kumnyakua binti huyo imekuwa ngumu hadi kumpelekea kuamua kunyoosha mikono juu.

Rapa huyo amefunguka kwamba ameamua mwenyewe kuachana na binti huyo wa Barack Obama kutokana na kushindwa kumpata hadi sasa.

Malia Obama
Malia Obama

Mwanamuziki huyo ameonesha kuvutiwa kimapenzi na binti mkubwa wa aliyekuwa Rais wa Marekani, Barack Obama, Malia Obama na kusema kama wangekuwa pamoja angemuhudumia ipasavyo.

Malia Obama ni mtoto wa kwanza wa Obama na Michel Obama ambapo amekuwa na ulinzi mkali licha ya baba yake kutoka madarakani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *