Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Frederick Sumaye amefunguka na kusema licha ya mambo anayofanyiwa na serikali ikiwa pamoja na kunyang’anywa mashamba yake lakini hawezi kurudi CCM.

Sumaye amedai kuwa toka alipohama chama hicho na kuingia upinzani wapo viongozi walitamka wazi kuwa dawa yake ni kupokonywa mali zake mpaka awe masikini na kudai hayo mambo ndiyo yameanza lakini hayawezi kumfanya kurudi tena katioka chama hicho.

Aidha Sumaye amekiri kuwa mashamba hayo aliyapata kwa njia halali na siku zote amekuwa akiyalipia kwa muda wote huo na kusema mashamba yake yeye amekuwa akiyaendeleza tofauti na inavyoelezwa kuwa mashamba hayo hayaendelezwi.

Serikali imetangaza kuchukua mashamba mbalimbali ya wananchi ambayo hayajaendelezwa kwa muda mrefu na wamiliki wa waeneo hayo, jambo ambalo limemkuta na Mhe. Sumaye kwa mashamba yake mawili kudaiwa kuchukuliwa na serikali kwa kigezo hicho hicho kuwa hayajaendelezwa kwa muda mrefu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *