Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye ameiomba serikali kusimamia misingi ya demokrasia katika kutatua malalamiko ya wananchi na kusimamia ustawi wa jamii ya Watanzania.

Sumaye ametoa kauli hiyo jana Jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa kama serikali itafanyia kazi malalamiko na mapendekezo yanayotolewa na wananchi ni wazi taifa litafikia malengo yake.

Sumaye ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Democrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Pwani amesema kuwa iwapo serikali itawasikilza wananchi hali hiyo inaweza kupunguza umasikini na kuongeza pato la taifa kwa ujumla.

Pia Sumaye amewaasa watendaji wa serikali kutumia vizuri misaada inayotolewa na nchi wahisani ili kuhakikisha fedha za wananchi zinazotumiwa katika ulipaji wa madeni hayo zinakuwa na manufaa kwa watanzania wote hasa wale wasiofikiwa na huduma muhimu za kijamii.

Sumaye amesema hayo kutokana na hali ya siasa inavyoendelea nchini kutoka kwa viongozi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *