Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Pwani, Frederick Sumaye, ameahirisha mkutano wa waandishi wa habari ulioandaliwa kwa ajili ya kumkabidhi rasmi kadi ya chama hicho Wema Sepetu.

Tukio hilo lilipangwa kuhitimisha tangazo la wema miezi kadhaa iliyopita kujiondoa Chama cha Mapinduzi(CCM) na akijiunga na Chadema.

Akizungumza na waandishi leo wakati akitangaza kuahirisha mkutano huo, Sumaye, amesema tukio hilo limeahirishwa kwa sababu Wema ameshindwa kufika kutokana na kubanwa na ratiba za Mahakama.

Wema anakabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kulevya aina ya bangi ambayo ilipangwa kuanza kusikilizwa leo.

Sumaye aliyekuwa amengozana na Mwenyekiti  wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha), Halima Mdee na Makongoro Mahanga, alisema Wema angekabidhiwa kadi na kuzungumza sababu za kujiunga Chadema.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *