Aliyekuwa waziri mkuu katika Serikali ya awamu ya tatu, Frederick Sumaye amesema kuwa licha ya kukatazwa kuzungumzia masuala ya siasa hawatanyamaza kuzungumza.

Sumaye amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kudai kuwa kuwa wataendelea kufanya kazi kwa niaba ya wananchi ambao wana imani nao.

Sumaye ambaye ni mwenyekiti wa Chadema kanda ya Pwani amesema kuwa nchi  kwasasa inakazana kujenga mfumo wa demokrasia kandamizi ambayo kwa kiasi kikubwa inarudisha nyuma maendeleo.

Amesema licha ya juhudi hizo za kuwarubuni baadhi ya viongozi wakiwamo madiwani wachache, hawatadhoofika na wataendelea kufanya kazi.

Sumaye amesema kwamba  wanataka kujenga upinzani  wa kweli wenye lengo la kusaidia wananchi.

Amesema katika kulihakikisha hilo hadi kufikia mwaka 2018 hakutakuwa na kijiji, mtaa utakaokuwa hauna tawi la Chadema.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *