Aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Frederick Sumaye amesema kunyang’anywa mashamba yake si sababu ya yeye kufikiria kurudi CCM.

Sumaye amesema hayo leo mbele ya waandishi wa habari baada ya mashamba yake ya Mabwepande na Morogoro kufutiwa hati ya umiliki kutokana na kutoendelezwa kwa mashamba hayo.

Amesema kuwa kunyang’anywa mashamba yake anajua ni uamuzi wa juu lakini haumdhoofishi afikirie  kurudi CCM.

Sumaye amesema kuwa mashamba yake yaliyofutwa na Serikali yalikuwa yanalipiwa kodi na yalikuwa yanamilikiwa kisheria.

Sumaye ambaye ni mwenyekiti wa Chadema kanda ya Pwani amesema kuwa wanataka arudi CCM lakini yeye ataki kurudi CCM kwanini wanamlazimisha arudi huko.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *