Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Chadema), amewataka wanasiasa kutowatumia vibaya wasanii kwa manufaa yao binafsi.

Amesema Bashite ni mtu aliyekataliwa na jamii, hivyo wasanii wasikubali kutumika kumsafisha.

Ameyasema hayo jana Bungeni Mjini Dodoma alipokuwa akisoma hotuba ya kambi rasmi ya upinzani kuhusu Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo.

Sugu amemtaka msanii Roma kujitokeza hadharani kusema ukweli ni kipi kilichotokea na ni nani aliyehusika katika tukio hilo la utekwaji wake na wenzie.

“Wanasiasa tunatakiwa tuwaheshimu wasanii kwani ni kioo cha jamii, kuwatumia na kuwaterekeza mtakuwa hawatendei haki,”.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *