Makamu wa Rais wa Sudan Kusini, Taban Deng Gai amekiri kuwa machafuko yaliyoibuka miezi ya hivi karibuni yamezorotesha uchumi kwa kiwango kikubwa hali iliyopelekea taifa hilo kuwa katika hali ya umasikini mkubwa.

Taban Deng Gai ameyasema hayo wakati akilihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa katika mkutano wake wa 71 unaoendelea mjini New York huku akisema serikali imeshaanza kuchukua hatua kuimarisha uchumi wa taifa hilo.

Gia amesema kile ambacho kinafanyika kwa sasa ni kuimarisha sera za fedha, kuimarisha kipato kitokanacho na mafuta, kujihusisha na shughuli za kilimo, madini, utalii ikiwa ni pamoja utalii wa mazingira na kuhamasisha watalii kuja Sudan Kusini.

Bwana Gai amesema kwamba utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDG’s unatekelezwa kwa ubia na nchi kama vile Kenya ,Uganda na Ethiopia kwa kuhakikisha kwamba kipaumbele kikiwa ni ujenzi wa miundombinu ya msingi kama vile barabara na nishati ili kuinua kiwango cha maisha ya raia.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *