Serikali ya Sudan Kusini imesema kwamba haijaandika barua inayosambazwa katika mitandao ya kijamii ikiamrisha jeshi la taifa hilo kumkamata aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar akiwa hai ama akiwa amefariki.

Msemaji wa serikali ya nchi hiyo alionekana katika runinga ya taifa na kutoa kile alichokitaja kuwa sababu saba kwa nini barua hiyo ni bandia ikiwemo ile ambayo inaenda kinyume na ukomeshaji wa uhasama uliokubalika.

Barua: Iliyosambaa ikiamlisha kukamatwa kwa Rieck MacharBarua: Iliyosambaa ikiamrisha kukamatwa kwa Riek Machar

Barua hiyo haina nambari za uthibitisho,uhalisi wa saini mbali na muhuri wa ‘siri’ kama ilivyotarajiwa, mtu  mmoja aliituma kanda ya video katika mtandao wa Facebook akiisoma taarifa hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *