Nchi ya Sudan Kusini imewaua wanajeshi wake 2 kwa kuwapiga risasi baada ya kupatikana na hatia ya kuwauwa wanandoa wawili ikiwa ni kisa cha kwanza cha mauaji kulingana na vyombo vya habari.

Wanajeshi hao walipigwa risasi mbele ya gwaride la kijeshi katika mji wa Wau Kaskazini Magharibi,huku wakaazi na familia za wanajeshi hao zikikongamana katika eneo hilo kuona mauaji hayo.

Mahakama ya kijeshi iliwapata na hatia wanajeshi, Meja Atian Deng na Matem Ariic Mayom kufuatia kukamatwa kwao mwezi Julai 17 mwaka huu katika ene la wakaazi la Wau.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *