Mshambuliaji wa Barcelona, Luis Suarez ameweka wazi nia ya kukatia rufaa kadi nyekundu aliyoonyeshwa kwenye mechi ya nusu fainali dhidi ya Atletico Madrid.

Suarez aliyefunga bao muhimu lililoisaidia Barcelona kutoka suluhu ya 1-1 na Madrid kwenye mchezo wa jana usiku alionyeshwa kadi nyekundu kwa kumpiga kiwiko kiungo wa Madrid, Koke.

Barca imefanikiwa kutinga fainali kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2.

Hii ni kadi ya kwanza nyekundu kwa mshambuliaji huyo wa Uruguay ndani ya kipindi cha miaka mitatu alichopo Catalan.

Hata hivyo kocha wa Barca, Luis Enrique ameweka wazi kuwa hana imani ya kuwa na mshambuliaji huyo kwenye mechi ya fainali ambapo watakutana na ama Alaves au Celta Vigo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *