Mshambuliaji wa Barcelona, Luis Suarez amesema kuwa timu yake itaifunga PSG kwenye mechi ya marudiano katika uwanja wa Nou Camp na kufuzu hatua ya robo fainali ya michuanao hiyo.

Barcelona walifungwa 4-0 na klabu ya Paris St- Germain katika hatua ya kwanza wa hatua ya 16 bora siku ya Jumanne.

Barcelona imeshinda kombe la Ulaya mara tano na wamefanikiwa kufuzu katika robo fainali mara tisa mfululizo.

Alipoulizwa kuhusu kocha wa klabu hiyo Luis Enrique ambaye kandarasi yake inakamilika mwishoni mwa msimu huu,Suarez alisema ”sote tunapaswa kulaumiwa”.

Barcelona ambayo iko katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa la liga na pointi moja nyuma ya viongozi Real Madrid wanakabiliana na Legannes nyumbani siku ya Jumapili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *