Kiungo wa kimataifa wa Scotland,  Darren Fletcher amejiunga na klabu ya Stoke City akitokea West Bromwich Albion.

Fletcher mwenye umri wa miaka 33 amejiunga na Stoke City kwa mkataba wa miaka miwili kwa uhamisho huru baada ya kumaliza mkataba wake na West Bromwich Albion.

Kiungo huyo kutoka nchini Scotland alijiunga na West Bromwich Albion mwaka 2015 akitokea Manchester Utd, baada ya meneja kwa wakati huo Louis Van Gaal kumuondoa kwenye mipango yake.

Msimu uliopita Fletcher aliichezea West Bromwich Albion michezo yote 38 ya ligi kuu England akifunga mabao mawili na kutengeneza mengine matatu.

Kusajiliwa kwa Fletcher huko Stoke On Trent, kunaibua hisia kabambe miongoni mwa mashabiki wa ligi ya nchini England ambao wanaamini safu ya kiungo ya Stoke City imepata mtu mkomavu ambaye ataweza kusadia kufikia malengo ya meneja Mark Hughes.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *