Staa wa RnB Bongo, Steve amefunguka kwa kusema kuwa hakupata mafanikio toka aanze kuimba kutokana na uongozi wake kushindwa kumsimamia vizuri.

Steve RnB ambaye alitoka kumuziki kupitia wimbo wa ‘Tabasamu’ aliyoshirikishwa na Mr Blue amesema kuwa uongozi wake huo hakumfanyika haki kipindi unamsimamia kwani hakupata mafanikio yoyote.

Mkali huyo amesema kwa sasa ameshamaliza mkataba na uongozi aliokuwa nao hapo awali na yupo kwenye mazungumzo na uongozi mwingine na kwamba mambo yakikaa sawa atarudi tena kimuziki na kurudisha hadhi yake aliyokuwa nayo hapo nyuma.

Pia Steve amewaahidi mashabiki wake kwamba anajipanga kurudi upya ili kuwapa mashabiki zake ngoma kali na pia kutoa nyimbo mara kwa mara ili mashabiki zake wasimkose kwenye game la Bongo fleva.

Steve RnB ni mwanamuziki nyota aliyejizolea sifa kutoka kwa mashabiki kutokana na vibao vyake kuwakonga mashabiki hao wa muziki wa Bongo felva kama vile One Love aliyomshirikisha Baby Boy na nyingine kibao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *