Muigizaji na mchekeshaji wa Bongo Movie, Steve Nyerere amesema kuwa Nay wa Mitego alikuwa sahihi kuwakosoa wasanii wa filamu walioandamana kupinga uingizwaji wa filamu kutoka nje ila alitumia lugha isiyo sahihi.

Steve Nyerere amesema kwamba yawezekana  Nay wa Mitego alikuwa na hasira hivyo akashindwa kutumia lugha sahihi ya kuwaelekeza wasanii wenzake walivyokuwa wanakosea ndio maana alitoa lugha yenye maneno makali ijapokuwa alikuwa sahihi kukosoa maandamano yale.

“Kwanza naomba nimuombee msamaha ndugu yangu Nay wa Mitego, hakuwa na nia mbaya lakini hakutumia maadili kufikisha ujumbe wake, Unajua sisi watanzania hatupendi kuambiwa ukweli na hata tukisemana tuna lugha zetu laini za kusemeshana”.

Pia ameongeza kwa kusema kuwa “Nay wa Mitego mpaka kutoa maneno makali vile ujue anaipenda tasnia yetu ya filamu alikuwa kaaumia, si unajua hata yeye alishawahi kuwa huku anatuonea huruma na anatupenda mimi niseme mumsamehe tuu”.

Muigizaji huyo ameongeza kuwa kwa hali ilivyo katika tasnia ya filamu Tanzania hakuna haja ya maandamano pamoja na kurushiana maneno kwenye mitandao bali kinachotakiwa ni kukalishana chini waigizaji wote na kuangalia mahali walipojikwaa na kufanya marekebisho.

.

 

 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *