Muigizaji wa Bongo Movie, Steve Nyerere amesema kuwa hakuna msanii hata mmoja ambaye anakidai Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Steve amesema kuwa mambo ambayo amesema Wema Sepetu kuwa anakidai chama hicho ni uongo na uzushi mtupu alioamua kuoneza ili kukichafua chama hicho tawala.

Kauli hiyo ya Steve Nyerere inakuja kufuatia Wema Sepetu kusema anakidai chama cha Mapinduzi pesa ambazo walimuahidi kumlipa wakati akikifanyia kampeni kwenye uchaguzi wa mwaka 2015.

 

Steve Nyerere amesema katika wasanii mbalimbali ambao huenda walilipwa pesa nyingi zaidi ni Wema Sepetu pamoja na yeye na kusema wao pamoja na wasanii waliokuwa wanaendesha kampeni ya Mama ongea na mwanao ni wasanii ambao walilipwa vizuri sana na Chama Cha Mapinduzi kuliko wasanii wengine wowote wale. 

 

Pia amesema katika mkataba walioingia na Chama Cha Mapinduzi hakuna sehemu mkataba huo unasema ukikamatwa na madawa ya kulevya, bangi kuwa chama hicho kitakuja kukusaidia.

 

Pia Steve Nyerere anakiri wazi kuwa sauti ambayo inazunguka kwenye mitandao ya kijamii ni kweli ni sauti yake na alikuwa akiongea vile ili kumridhisha mama yake na Wema Sepetu kwani wakati huo jambo hilo lilikuwa ngumu kwake. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *