Muigizaji wa vichekesho nchini, Steve Nyerere amewataka watu kuacha kumuhusisha kwenye sakata la kutengeneza audio ambayo anasikika Wema Sepetu akizungumza mambo ya faragha na Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA, Freeman Mbowe.

Steve Nyerere amedai kila mtu anajua hawezi kufanya kitendo kama hicho kwaajili ya kumchafua mtu bali wanataka kumchafua.

Pia sema hataki kulizungumzia zaidi sakata hilo kwa kuwa anaweza akaanzisha mjadala mpya kitu ambacho hapendi kitokee.

Muigizaji huyo alihusishwa kwenye tukio hilo baada ya kusikika mtu anayedaiwa kuwa ni Wema akitaja jina lake.

Kwa upande wa Mbowe aliikataa audio hiyo kwa kusema siyo yake huku akiwataka Wanzania kutulia wakati timu yake ikifanya uchunguzi juu ya sakata hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *