Meneja wa Hull City, Steve Bruce amehojiwa na Chama cha soka nchini Uingereza ”FA” kuhusu kupewa kazi ya kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Uingereza.

Vile vile kocha wa Sunderland, Sam Allardyce ameshahojiwa na ‘FA’ kwa ajiri ya kupewa kazi hiyo kuchukua nafasi ya kocha Roy Hodgson ambaye amejiuzuru baada ya kufungwa dhidi ya Iceland kwenye mashindano ya Euro mwaka huu.

Bruce mwenye miaka 55 ameiongoza Hull  City kurejea kwenye ligi kuu chinini Uingereza msimu ujao baada ya kushuka 2015.

Kwa upande mwingine kocha wa Bournemouth, Eddie Howe na kocha wa Marekani, Jurgen Klinsmann pia wamehusihwa katika kuchukau nafasi hiyo.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *