Mkali wa hip hop nchini, Stereo ametoa pongezi kwa rapa mwenzake Nikki wa Pili kwa kuendelea na PHD huku na yeye akifuata nyayo zake kwa kusema anataka kwenda kuchukua elimu ya PHD pia.

Stereo amesema kuwa kwa sasa ana elimu ya degree lakini hatasita kuitafuta elimu ya PHD huku akimpongeza Nikki wa Pili kwa kuweza kuwa chachu kwa wasanii wengine akiwemo yeye kutamani kusonga mbele kielimu.

Nikki wa Pili
Nikki wa Pili

Hata hivyo Stereo amemalizia kwa kuwashauri wasanii wenzake kujipanga vyema hasa katika maswala muhimu ya elimu kwa kuwa elimu inasaidia sana hata katika maswala ya muziki wao kwa kuwa muziki ni biashara ambayo inakuwa kwa kasi sana.

Nikki wa pili kwasasa anaendelea na elimu ya PHD jambo ambalo limemgusa mwanamuziki Stereo na yeye kutaka kuendelea na elimu hiyo ya PHD.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *