Mchezaji tennis namba nne kwa ubora upande wa wanaume, Stan Wawrinka amejiondoa kushiriki michuano ya Olimpiki.

Mchezaji huyo amejiondoa kushiriki mashindano hayo makubwa duniani baada ya kupata majeraha katika michuano ya Rogers Cup iliyofanyika huko Toronto, Canada.

Nyota huyuo aliondolewa katika hatua ya nusu fainali baada ya kufungwa na Kei Nishikori mwezi uliopita na kutokana na ushauri wa daktari wake ameamua kujiondoa katika michuano hiyo.

Wachezaji wengi mashuhuri wa mchezo huu wa tenesi wamejiondoa kushikiri michuano hiyo akiwemo Roger Federer, Marcos Baghdatis kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *