Comedian maarufu nchini, Stan Bakora amesema kuwa sababu ya kupakaa masizi kwenye video aliyoifanya ya wimbo wa Nisamehe wa Baraka The Prince ni kuleta uhalisia wa video hiyo.

Mchekeshaji huyo amesema kuwa kama asingefanya vile kwenye video hiyo ingekuwa ya kawaida tu na isingeleta maana katika jamii na watu wangeona kama amerudia nyimbo ya Baraka.

Stan aliendelea kusema kuwa kama asingefanya vile ile video isingeleta maana, lazima uonyeshe uhalisia kwani Baraka si mweusi kweli?,”.

Awali baada ya Stan kuachia video hiyo, Barakah aliandika kwenye ukurasa wake Instagram: Matani ni mazuri ila yakizidi yanaweza kuleta matatizo… heshima ichukue nafasi yake tafadhali mzee utani huu sijaupenda iwe mwanzo na mwisho tafadhali.”

Kutokana na kilichotokea kwa wawili hao kumeleta marumbano baina yao kwasababu Baraka anadai amedharirishwa na Stan Bakora kwa kitendo chake cha kujipaka masizi ili afanane naye ili kuleta uhalisia wa video hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *