Staa wa Hip Hop nchini, Stamina amesema kuwa anatarajia kuachia albam yake mpya ifikapo Disemba mwaka huu huku akibainsha kwamba albam hiyo itakuwa na nyimbo 15.

Stamina amesema tayari ameshamaliza kurekodi nyimbo zote za albamu hiyo na sasa ipo katika hatua za mwisho za maandalizi ya kutoka.

Rapa huyo amesema “Albamu mpya kwa sasa ipo jikoni kwa Rash Don, nimeshamaliza kurekodi na Disemba inaingia sokoni,”.

Stamina aliendelea kusema kuwa “Nashukuru mungu hii ni tofauti ili iliyopita, mapaka sasa ninapozungumza na wewe tayari kuna wadhamini wamejitokeza kwa ajili ya usambazaji pamoja na kuandaa matamasha ya uzinduzi,”

Staa huyo kutoka mkoani Morogoro amesema nyimbo hizo 15 amefanya na maproducer tofauti tofauti ili kupata ladha katika kila wimbo.

Stamina hadi sasa ameshatoa albam moja iliyojuliakana kwa jina la ‘Mt Uluguru’ ambayo ilifanikiwa kuuza nakala iliuza 9,000.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *