Klabu ya Singida United leo imeingia mkataba wa mwaka mmoja na kampuni ya SportPesa wenye thamni ya milioni 250.

SportPesa imeendelea kuonesha dhamira katika kuhakikisha Ligi Kuu soka Tanzania bara msimu ujao 2017/2018 kunakuwa na ushindani wa kweli kutoka katika timu mbalimbli kutokana na jitihada zake za kudhamini vilabu kadhaa.

Kampuni hiyo imetangaza kuingia mkataba wa mwaka mmoja wa udhamini na klabu hiyo ya Singida United ya Singida wenye thamani ya Tsh milioni 250.

Singida United imepanda Ligi Kuu Tanzania bara msimu huu na itashiriki Ligi Kuu msimu ujao wa 2017/2018.

Mkataba huo umekuja baada ya kuingia mkataba wa udhamini na Simba na Yanga katika kipindi cha miaka mitano wenye thamani ya zaidi ya Tsh Bilioni 4.

Picha kwa hisani ya Global Publishers

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *