Spika wa Bunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amewataka vijana nchini kugombea nafasi mbalimabali  za uongozi ikiwemo udiwani na ubunge ili kutatua tatizo la kukosa ajira kutokana na kukosa uzoefu.

Spika Ndugai amesema hayo Bungeni leo baada majibu ya Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Bunge, Jenista Mhagama, kutokana na swali la mbunge wa viti maalumu Zainab Katimba aliyetaka kujua mkakati wa Serikali katika kutatua tatizo la ajira kwa vijana wasomi wasikuwa na uzoefu.

“Asante sana Waziri wa nchi kwa majibu ya nyongeza, Vijana wasomi, zipo kazi nyingine hazihitaji uzoefu, mnaweza mkagombea Udiwani, mkagombea Ubunge, nawatangazia vita waheshimiwa hapa” amesema Spika Ndugai.

Awali Naibu Waziri, Sera, Bunge, kazi, vijana, ajira  na walemavu Anthony Mavunde amesema kwamba serikali imeendaa utaratibu wa kuwapa vijana nafasi za kujitolea katika makampuni na mashirika mbalimbali ili kupata uzoefu wa kuweza kuajiliwa

Amessema “Kupitia mpango huu utawasaidia sana vijana wasomi  wa nchi yetu ambao walikuwa wakipata tabu na kikwazo cha uzoefu, kwa hivi sasa atapata nafasi ya kujifunza katika kampuni kwa muda huo wa mwaka mmoja na badae tutampatia cheti cha kumtambua ili iwe kama kiambatanisho chake”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *