Spika wa Bunge, Job Ndugai ameagiza kutafutwa kwa Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea na apelekwe kesho kwenye Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama ili ahojiwe kuhusu kauli aliyoitoa ya kumtuhumu Spika kuwa amedanganya idadi ya risasi alizopigwa Tundu Lissu.

Pia  Spika Ndugai ameagiza Kubenea na Mbunge wa Kigoma Mjini(ACT Wazalendo), Zitto Kabwe kupelekwa katika Kamati ya Bunge ya Maadili na Madaraka kwa tuhuma mbili tofauti

Zitto anatuhumiwa kutamka kuwa Bunge limewekwa mfukoni na muhimili fulani, wakati Kubenea ni kwa kumtuhumu Spika kusema uongo wa idadi ya risasi alizopigwa Lissu.

Spika Ndugai ametoa maagizo hayo bungeni mjini Dodoma leo wakati vikao vya Bunge hilo vinavyoendelea mkoani humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *