Mshindi wa Tuzo ya Nobel na mwandishi raia wa Nigeria, Wole Soyinka amesema kuwa ataondoka Marekani siku ambayo Donald Trump ataapishwa kuwa rais.

Wiki iliyopita Soyinka aliahidi kuwa angechana green Card yake ikiwa Trump angechaguliwa kuwa rais wa Marekani.

Green Card humpa mtu kibali ya kuishi rasmi nchini Marekani na hupewa umuhimu mkubwa na wahamiaji kutoka nchi za Afrika.

Soyinka ametoa matamshi hayo wakati akihutubia wanafunzi katika chuo cha Oxford nchini Uingereza.

Mwandishi huyo maarufu alionekana kuchukua msimamo mkali kupinga seza za uhamiaji za bwana Trump.

Soyinka alishinda tuzo ya Nobel la fasihi mwaka 1986 na kuwa mwafrika wa kwanza kupata tuzo hiyo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *