Klabu ya Southampton jana imeizamisha Liverpool kwa goli 1-0 kwenye mechi ya nusu fainali ya kwanza michuano ya kombe la ligi (EFL) iliyofanyika katika uwanja wa St Mary.

Goli la ushindi la Southampton limefungwa na Nathan Redmond katika dakika 20 ya mchezo huyo baada ya kumalizia vizuri pasi ya Jay Rodriguez na kuifanya Southampton kuongoza hadi kipindi cha kwanza cha mchezo huo.

Kipindi cha pili kilipoanza Liverpool walionyesha nia ya kurudishwa goli lakini wakshindwa kutokana na aina ya mchezo wa mchezo wa Southampton waliokuwa wanaucheza ni wa kukaba kwa hiyo mpaka mchezo unamalizika matokeo yalikuwa 1-0.

Mchezo wa marudiano unatarajiwa kuchezwa katika uwanja wa Anfield mnamo Januari 25 mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *