Mwenyekiti wa Umoja wa Wanwake Tanzania (UWT), Sophia Simba ametangaza kutogombea tena nafasi hiyo kwenye uchaguzi wa Chama hicho unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na  wanawake wa umoja huo wakati wa maadhimisho ya wiki ya wanawake Duniani yaliyofanyika jijini Dar es salaam.

Sophia Simba ametaja sababu zilizomfanya asigombee kuwa ni azma yake ya kuutumikia umoja huo kwa muda wa vipindi viwili tu na si zaidi ya hapo.

Pia amesema kuwa akiwa ndani ya UWT amebahatika kushika nafasi mbalimbali za uongozi kwa sababu alianzia nafasi ya ukatibu wa tawi la Kaskazini NDC.

Hata hivyo amesema kuwa anamshukuru mungu kwa kumjalia kushika nafasi mbalimbali kwa kuwa amekuwa mbunge kwa muda wa miaka 22.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *